Urusi yajiondoa katika mkataba wa silaha hatari

Rais Vladimir Putin amesema Urusi itaanza kuunda makombora mapya

Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi.

Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya.

Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake siku ya Ijumaa

Mkataba huo uliyofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.

"Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi''.

Urusi imekuwa ikikanusha tuhuma za kukiuka mkataba wa vita baridi.

Rais wa Putin aidha amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu