Miaka 2 baada ya kufariki Etienne Tshisekedi, Je sasa atazikwa DR Congo?

February 2, 2019

Ni miaka miwili sasa tangu kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Etienne Tshisekedi afariki dunia mjini Ubelgiji, lakini mpaka sasa mwili wa marehemu babake rais mpya wa DRC, Felix Tshisekedi hauja rejeshwa nchini.

Familia yake na chama chake, zilituhumu kwamba rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila amezuia juhudi za kurejeshwa kwa kiongozi huyo wa kisiasa nchini.

Leo imetimia miaka miwili, mwili wa marehemu Etienne Tshisekedi wa Mulumba umesalia ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti huko Ubelgiji.

Licha ya juhudi za familia yake na chama chake kutaka mwili wake urudishwe nchini Congo, serikali, chama na familia yake zilikosa kueleweana kuhusu pahala pa kumzika marehemu

 

Chama chake UPDS kilitaka azikwe katika makao ya chama, lakini serikali ilikataa na badala yake awali iliagiza azikwe katika makaburi yaliopo kwenye mtaa wa Gombe, na baadae walikubaliana azikwe katika kiwanja cha familia yake kilichokuwa mbali na mji wa Kinshasa, lakini mipango yote yalisitishwa

Felix Tshisekedi (pichani) rais wa sasa DRC ni mwana wa waziri mkuu wa zamani na muasisi wa muungano wa upinzani wa UPDS -Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini Brussels mwezi wa Februari 2017

Kwa mujibu wa familia ya marehemu , hadi sasa mjane, mkewe marehemu Tshisekedi hajatoka nje kwa muda wa miaka miwili sasa, hata siku alipoapishwa mwanawe Felix Tshisekedi, hakuweza kufika kulingana na mila ya familia hiyo ambayo hairuhusu mjane kusafiri au kufanya shuguli zozote wakati mwili wa mpenzi wake hauja zikwa.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon