Tumesalia bila chochote isipokuwa ndoto zetu:Wakimbizi wa Palestina


Atef A-nimnim na familia yake katika kambi ya wakimbizi wa kipalestina walioko Gaza.

Maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina wanaoshi Ukanda wa Gaza wanasema hawana chochote, hata matumaini yameanza kupotea isipokuwa ndoto zao. Hii ni kutokana na madhila na machafuko ya miaka nenda rudi katika eneo hilo linalokaliwa na Israel. Wengi wanaishi makambini ikiwemo kambi ya Al-Shati.

“Angalia chumba hiki, angalia mlango mvua inaponyesha nyumba inafurika, Watoto wangu wote wanalala hapa, mtoto wangu wa kiume ana miaka 27 analala nje ya chumba, na mwingine wa kiume wa miaka 18 analala jikoni,

hali nyumbani kwangu ni nimekuwa nikiteseka kwa zaidi ya miaka 20.” Anaitwa Atef A-nimnim akielezea maisha yake na namna anavyoishi na familia yake katika kambi ya wakimbizi nchini Palestina.

Licha ya adha hiyo hofu kubwa ya Umm si malazi, bali ni wanae, mkubwa wa kiume anataka kuondoka Gaza na mvula mdogo ana ndoto za kwenda kusaka maisha bora kwa ajili yake na familia yake nje ya Gaza.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu