HRW - Unyanyasaji wa wanaharakati wa amani waongezeka Myanmar


Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch imesema serikali ya Myanmar chini ya mshindi wa tuzo ya kimataifa ya Nobel Aung San Suu Kyi ilitumia sheria kandamizi kuwashitaki wanaharakati.

Ripoti hiyo ya Human Rights Watch imesema uhuru wa kujieleza umezidi kudhoofika tangu utawala wake ulipoingia mamlakani mnamo mwaka 2016, katika wakati ambapo mashitaka yakiibua kile ilichokiita "mazingira ya hofu" miongoni mwa waandishi wa habari.

Mshauri wa masuala ya sheria wa Asia katika shirika hilo, Linda Lakhdhir amesema kwenye taarifa yake kwamba Aung San Suu Kyi pamoja na chama chake cha National League for Democracy waliahidi Myanmar mpya, lakini serikali yake bado inatuhumu hotuba na maandamano ya amani na imeshindwa kurekebisha sheria kandamizi za zamani.

Hata hivyo msemaji wa serikali hakupatikana mara moja kujibu tuhuma hizo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya kijeshi inayotawala Myanmar kwa miongo kadhaa imeweka sheria kali dhidi ya uhuru wa kujieleza.

Marekebisho yaliyofanywa na serikali ya kiraia iliyoingia mamlakani mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kufutiliwa mbali kwa udhibiti, kulisababisha matokeo chanya katika masuala ya uhuru wa habari na hata mikusanyiko.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu