Mahatma Gandhi anauawa na Mhindu mwenye itikadi kali 1948


Tarehe 30 Januari 1948 Mahatma Gandhi anauawa na Mhindu mwenye itikadi kali anayechukia jitihada za Ghandi za kutunza umoja wa Uhindi na kutetea haki za Wahindi Waislamu.

Wakili Gandhi mwaka 1906 katika Afrika Kusini

Gandhi alizaliwa katika eneo la Gujarat kama mtoto mdogo wa Karamchand Gandhi na mama Putali Bai. Baba yake alikuwa waziri mkuu katika serikali ya maharaja wa nchi lindwa ndogo ya Porbandar wakati ilipokuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza.

Familia yake ilifuata dini ya Uhindu madhehebu ya Wavishnu lakini nyumba ya Gandhi ilitembelewa pia na Waislamuna Wajain.

Gandhi na Kasturba mnamo 1902

Mwaka 1883 akiwa na umri wa miaka 13 aliozwa kwa mke wake Kasturba wakazaa watoto 4.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu