Marekani yaishtaki Huawei kwa madai ya wizi wa teknolojia

'Kwa miaka sasa kampuni za China zimekiuka sheria za biashara ya kimataifa'-Marekani.

Marekani imeishtaki kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei na afisaa mkuu wake wa fedha, Meng Wanzhou.

Mashataka hayo ni pamoja na ubadhirifu wa fedha, kupinga utekelezaji wa haki na wizi wa teknolojia. Kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China hali ambayo itaathiri biashara ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei imekanusha madai hayo.

Katika taarifa, Huawei imesema kuwa "imeghadhabishwa na mashtaka dhidi ya yake".

Imesema kuwa haikufanya makosa yote "yanayodaiwa ilitekeleza" na kwamba"haina ufahamu wa kosa alilotekeleza Bi Meng".

Meng ambaye ni binti wa mwanzilishi wa Huawei, alikamatwa nchini Canada mwezi uliyopita kufuatia ombi la Marekani kwa madai ya kukiuka vikwazo vyake dhidi ya Iran.

"Kwa miaka sasa, kampuni za China zimekiuka sheria zetu za biashara ya kimataifa, hatua ambayo inahujumu vikwazo vyetu na mara nyingine kutumia mfumo wa fedha wa Marakani kuendesha shughuli zao haramu. Hili lazima likomeshwe," alisema waziri wa biashara wa Marekani, Wilbur Ross.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu