Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

UNICEF yatoa ombi la dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kusaidia watoto milioni 41duniani

January 29, 2019

Mamilioni ya watoto wanaoishi katika nchi zilizoathiriwa na mizozo na majanga wanakosa huduma muhimu za ulinzi na hivyo kuweka usalama na mustakabali wao hatarini, 

 limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia watoto, UNICEF huku likisema linahitaji ombi la dola bilioni 3.9 ili kusaidia katika shughuli zake kwenye majanga ya kibinadamu.

UNICEF katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi, Marekani, limesema linatarajia fedha hizo kusaidia watoto milioni 41 kwa mwaka 2019 ambapo fedha hizo zitatumika kusambaza maji safi na salama, lishe, elimu, huduma ya afya na ulinzi katika nchi 59 kote ulimwenguni.

Mathalani, dola milioni 385 kati ya ombi hilo, ni kwa ajili ya programu za ulinzi huku milioni 121 ni kwa huduma za ulinzi kwa watoto walioathirika kutokana na mzozo wa Syria.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore amesema, “leo mamilioni ya watoto wanaoishi katika mizozo na majanga wanakabiliwa na ukatili wa kusikitisha, dhiki na kiwewe na hatua chanya za kazi  yetu ya ulinzi wa watoto haiwezi kusisitizwa zaidi."

 UNICEF imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia katika ufadhili huku likionya kuwa ukata huenda ukasababisha baadhi ya watoto kuachwa nyuma katika nyanja mbali mbali.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload