Bata mpweke zaidi duniani afariki

January 28, 2019

Bata Trevor : Kisiwa cha Niue kinaomboleza kifo cha bata aliyekuwa peke yake nchini humo

Trevor, ambaye alikuwa akifahamika kama bata mpweke zaidi duniani amefariki baada ya kushambuliwa na mbwa kwenye kisiwa kimoja cha mbali kwenye bahari ya Pasifiki.

 

Trevor alikuwa maarufu sana kwenye kisiwa kidogo cha Niue kutokana na kuwa ndege pekee wa aina yake kuishi kwenye kisiwa hicho.

 

Aliwasili kisiwani hapo mwaka 2018, hata hivyo haijulikani ni kwa namna gani alifika kisiwani hapo.

 Alikuwa akiishi kwenye dimbwi lililokuwa pembezoni mwa barabara, na alikuwa akihudumiwa na kupewa chakula na wenyeji wa eneo hilo.

 

"Alionekana hapa Niue mwezi Januari 2018 baada ya kutokea gharika kubwa, tunaamini alipaa ama alipeperushwa mpaka kufika hapa," amesema Rae Findlay, mkuu wa chama cha wafanyabiashara wa Niue ambaye pia alifungua ukurasa wa Facebook wa bata huyo''

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon