Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mamia ya watu wahofia kufa baada ya bwawa kuvunja kingo zake nchini Brazil

January 27, 2019

Watu 200 hawajulikani waliko baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil.

Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyikazi wa shirika hilo.

 

Shughuli ya kuwatafuta manusura inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika jimbo la Minas Gerais.

Gavana wa jimbo hilo Romeu Zema amesema kuna hofu huenda watu wengi wamefariki katika mkasa huo.

Baadhi ya watu waliyokwama kwenye matope, waliokolewa kwa kutumia helikopta baada ya barabara kuharibiwa.

 

Watu wengine wamehamishiwa kutoka makaazi yao kutokana na sababu za kiusalama.

 

Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Vale, Fabio Schvartsman thuluthi moja ya wafanyikazi karibu 300 hawajulikani waliko.

 

"Nina hofu nataka kujua hali ni mbaya kiasi gani'' alisema Helton Pereira mmoja wa jamaa za watu waliyoathiriwa na mkasa huo''.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload