Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.01.2019: Mata, De Ligt, Otamendi, Berta, Suarez

January 25, 2019

Kiungo raia wa Uhispania Denis Suarez, 25, anataka kujiunga na Arsenal kwa mkopo, lakini klabu yake ya Barcelona inataka kumuuza kiungo huyo kwa timu za Sevilla ama Real Betis.

Denis Suarez

Klabu ya Barcelona imefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Juan Mata. Mata, 30, ambaye ni raia wa Uhispania atamaliza mkataba wake na United mwisho wa msimu huu.

Juan Mata

Manchester City wanataka kumsajili beki wa kati wa Ajax, Mholanzi Matthijs de Ligt, 19. Iwapo usajili huo utafanikiwa inatazamiwa beki raia wa Argentina Nicolas Otamendi, 30, anaweza kujiunga na Barcelona.

Matthijs de Ligt

 

Manchester United wana nia ya kumuajiri mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid Andrea Berta, lakini klabu ya Atletico imempa mkataba mnono afisaa huyo raia wa Italia.

Andrea Berta

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload