Waethiopia wanawashinda Waitalia katika mapigano ya Dogali-1887

Dogali, 1887

Dogali katika tambarare ya pwani ya Eritrea takriban 30 km kutoka Massawa ni mahali pa mapigano yaliyotokea tarehe 24 Januari 1887 kati ya wanajeshi wa Italia na Ethiopia.

Kikosi cha Waitalia 587 kilielekea kaskazini kutoka Massawa kikashambuliwa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus wa Ethiopia. Karibu Waitalia 500 waliuawa na 80 walijeruhiwa na kurudi.

Kuna kumbukumbu ya mapigano kwenye obeliski huko Roma na makaburi ya Waitalia waliokufa

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu