Agano la Amani la kusitisha Vita ya Vietnam lilitiwa sahihi mjini Paris-1973

January 23, 2019

  Ingawa Agano la Amani la kusitisha Vita ya Vietnam lilitiwa sahihi mjini Paris mnamo tarehe 23 Januari mwaka  1973 lakini  mapigano yakaendelea hadi mwaka 1975.

 

Vita ya Vietnam

Vita ya Vietnam ilikuwa vita iliyopigwa katika nchi ya Vietnam kati ya miaka 1960 na 1975 lakini mapigano yake yalienea hadi nchi jirani za Kambodia na Laos.

 Wakati ule Vietnam iligawiwa katika madola mawili ya Vietnam Kusini na Vietnam Kaskazini.

 Ilikuwa hasa vita ndani ya Vietnam Kusini. Kwa upande mmoja walisimama serikali ya Vietnam Kusini pamoja na askari za Marekani na nchi mbalimbali zilizoshikamana nao.

 kwa upande mwingine wanamgambo wa Vietkong pamoja na jeshi la Vietnam Kaskazini iliyosaidiwa na nchi za Kikomunisti kwa pesa na silaha.

 

Mapigano yalitokea hasa ndani ya Vietnam Kusini. Vietnam Kaskazini ilishambuliwa kwa mabomu ya ndege ya Marekani na wanajeshi wake walitumwa kupiga vita katika kusini.

 Vita ilikwisha kwa ushindi wa Vietnam kaskazini mwaka 1975

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon