Vikosi vya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini vinawapeleka wanafunzi shuleni wakati wa mitihani.


Walinda amani wa UNMISS wakishika doria katika barabra karibu na Bentiu, jimbo la Unity, Sudan Kusini.

Walinda amani Sudan Kusini wasindikiza wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.

Polisi waliopo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamepewa jukumu la kuwasindikiza wanafunzi hadi kwenye kituo cha mtihani kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba

Usindikizaji huo unafanyika Kwa wiki mbili ambapo askari hao wataendelea kuwapeleka na kuwarudisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa usalama.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS unasema ili safari iwe salama ni lazima kuwepo mipango ya kina, mathalani Afisa wa polisi na mwalimu wanatakiwa kuwa katika kila basi, njia ya kupita inapangwa na ulinzi unawekwa njiani na katika kipindi chote cha kufanya mtihani na eneo la shule.

Sarah Kerr,mmoja wa wanafunzi wanaofanya mitihani anasema, “tunajisikia fahari kwamba usalama umetuzunguka. Wametuleta hapa. Wanatutendea vizuri. Wanahakikisha mazingira ambayo tunafanyia mitihani yanafaa na salama. Ndiyo, hiyo ni safi, ninajikia furaha”

Baadhi ya wanafunzi hawa ambao ni miongoni mwa wanaoishi katika vituo vya ulinzi wa raia tangu mwaka 2013 wakati mgogoro ulipoanza nchini Sudan Kusini wana ndoto za kuwa wanasheria na viongozi na matumaini yao ni kuwa wataweza kuhakikisha kunakuwepo na amani ya kudumu na uatawala wa sharia katika nchi ambayo imeathirika na miaka mingi ya migogoro na mifumo iliyoharibika.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu