The Man-Eaters of Tsavo-1907


The Man-eaters of Tsavo ni kitabu kilichoandikwa na John Henry Patterson mnamo mwaka wa 1907 na kinaelezea maisha yake wakati alikuwa anajenga reli ya Uganda kupitia Kenya.

kwa wengi kitabu hiki kinayojulikana sana kwa kurekodi hadithi ya jozi ya simba ambao aliwaua wakati alikuwa nchini Kenya, ambao pia walikuwa wanajulikana kama wala watu wa Tsavo.

Kitabu hiki pia kina picha zilizochukuliwa na Patterson wakati huo ambazo zinajumuisha picha zilizopigwa wakati wa ujenzi wa reli; wafanyakazi; makabila ya Kenya; maonyesho maridadi na wanyamapori; na walaji binadamu ambao walikuwa simba.

Hadithi ya kitabu hiki imetumiwa katika filamu mara tatu: a monochrome, filamu ya Uingereza ya mwaka wa 1950, filamu ya mwaka wa 1952 ya 3-D ya iliyojulikana kama Bwana Devil l, na filamu ya mwaka wa 1996 toleo lililoitwa The Ghost and the Darkness ambapo Val Kilmer alicheza kama mhusika mkuu aliyekuwa mhandisi ambaye hakuwa na uoga wa kuwawinda simba wa Tsavo

Kitabu hiki kinaelezea mashambulizi ya simba waliokuwa wanawala binadamu ambao walikuwa wajenzi wa Reli ya Uganda katika Tsavo, Kenya mwaka wa 1898 na jinsi simba walivyo uwawa na mwandishi wa kitabu hiki, Patterson.

Hadithi hii ilikuwa ya ajabu kwani takriban watu 35 waliuawa na simba hao kwa muda wa chini ya mwaka mmoja kabla Patterson kuwaua (ingawa idadi hii inapingwa).

Kitabu hiki cha Patterson cha mwaka 1907 chenyewe kinasema kwamba " hakuna Wahindi walionusurika na kifo cha simba takribani 28, pamoja na Waafrika ambao kwa bahati mbaya waliuwawa na ambao walikuwa wenyezji wa sehemu hiyo "

Idaidi hii ndogo ilithibitisha katika kitabu cha Dk Bruce Patterson cha The Lions of Tsavo: Exploring the Legacy of Africa's Notorious Man-Eaters (McGraw-Hill, 2004),

Kufuatia vifo vya simba hawa, kitabu kinaelezea ukamilifu wa reli na vilevile hadithi nyinginezo nyingi kuhusu wanyamapori wa humo nchini Kenya (pamoja na simba wengine), makabila ya Kenya, ugunduzi wa pango ya walaji wanadamu, na uwindaji mbalimbali wa vikundi.

Kitabu hiki pia kinajumuisha nyongeza ambayo inatoa ushauri watalii wote ambao wanaitembelea Afrika Mashariki

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu