Francisco Pizarro anaunda mji wa Lima (Peru)-1535,[Mwanajeshi aliyekuwa hajui kuandika]

January 18, 2019

Tarehe 18 January mwaka 1535 Francisco Pizarro anaunda mji wa Peru 

 

Francisco Pizarro alikuwa conquistador (mwanajeshi) Mhispania aliyevamia Peru na kuharibu Dola la Inka mwaka 1533.

Pizarro alizaliwa 1471 (au 1478) mjini Trujillo (Hispania). Mwaka 1509 aliondoka Hispania kwenda Amerika katika koloni mpya za Hispania.

Pizarro hakujua kuandika akachora alama mbili tu na karani akaongeza maandishi ya jina

Alipokaa miaka kadhaa katika Panama Pizarro alisikia habari za nchi tajiri katika kusini iliyoitwa "Peru". Alifanya safari tatu akifuata mwambao wa Kolombia na Ekuador akafika katika mji wa Tumbes uliokuwa tayari sehemu ya Dola la Inka alipopokelewa vizuri

Francisco Pizarro mnamo 1540

 

Pizarro akarudi Hispania akajipatika kibali cha Kaisari Karolo V ya kuwa gavana wa Peru akifaulu kuvamia na kuteka nchi ile isiyojulikana hadi wakati ule kama angeweza kufaulu kwa gharama zake mwenyewe

 UVAMIZI WA PERU

 

1531 alitoka Panama kwa jahazi 3 na watu 207. Mwezi wa Agosti 1532 aliunda Piura kama mji wa kwanza wa Kihispania nchini Peru. Katika Septemba aliongoza jeshi lake kuelekea nyanda za juu katika milima ya Andes ambako alisikia angekuta mji mkuu wa Inka.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon