Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 17.01.2019: Higuain, Morata, Ozil, Batshuayi, De Jong

Manchester City huenda wakapoteza nafasi ya kumsajili Frenkie De Jong kutoka Ajax baada ya Paris St-Germain kuonyesha azma ya kutaka kumununua kiungo huyo.

Japo De Jong wa miaka 21 angelipendelea ujiunga city chini ya Pep Guardiola, PSG ndio klabu pekee ambayo iko tayari kulipa Ajax euro milioni 66.

Batshuayi anataka sana kukamilisha mkopo wake ili aweza kuhamia Monaco.

Gonzalo Higuain

Chelsea wameamua kumsajili Gonzalo Higuain baada ya Juventus kukubali ofa yao. Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa akichezea AC Milan kwa mkopo.

lvaro Morata,

Atletico Madrid wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Chelsea lvaro Morata, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 45.

Arsenal wako tayari kutumia sehemu ya mshahara wa Mesut Ozil endapo watafanikiwa kumuuza ili kumsajili mchezaji mwingine.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu