Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 14.01.2019: Wilson, Ake, Llorente, Neves, Arnautovic, Babel

January 14, 2019

Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhipania Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, analengwa na Barcelona

Fernando Llorente

Bournemouth iko radhi kumuuza mshambuliaji wa England Callum Wilson wa Chelsea kwa pauni £75m - mara 25 zaidi ya kiwango walicholipa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mnamo 2014.

 

 Callum Wilson

 

Chelsea pia inataka kumsajili upya beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake, miaka miwili tu baada ya kumuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Cherries.

Nathan Ake

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo haitofikiwa kiwango kinachohitajika kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves mwenye umri wa miaka 21 cha thamani kwa thamani ya £100m.

 Pep Guardiola

Winga wa West Ham Michail Antonio anasema mchezaji mwenza wa Hammers na mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, anataka kuelekea China.

 

Austria Marko Arnautovic

 

Aliyekuwa winga wa Liverpool Ryan Babel, mwenye umri wa miaka 32, anakaribia uhamisho kwenda Fulham kwa mkopo. Raia huyo wa Uholanzi kwa sasa anaichezea Besiktas.

Ryan Babel

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon