Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mjamzito aliyepona Ebola DRC ajifungua mtoto asiye na Ebola, madaktari wastaajabu!

January 14, 2019

Mhudumu wa afya anayehusika na ebola akimchunguza ugonjwa huo mtoto mchanga mwenye umri wa wiki moja kwenye hema maalum la kituo cha matibabu dhidi ya ebola huko Beni jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC Desemba 3, 2018.

 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC madaktari wamestaajabu baada ya mjamzito aliyepona ugonjwa wa ebola kujifungua salama mtoto wake ambaye hajaambukizwa ugonjwa virusi vya ugonjwa huo.

 WHO inasema kwa kawaida watoto wanaozaliwa na mama mwenye ebola mara nyingi huzaliwa tayari wameambukizwa ugonjwa huo na mara nyingi hufariki dunia.

Hata hivyo katika mlipuko huko Beni, kutokana na malezi kwa watoto wachanga, idadi kubwa wamepona na wanasema Sylvana ni mtoto wa kwanza kuzaliwa na manusura wa ebola bila kuwa ameambukizwa kirusi hicho. Dkt. Junior Ikomo kutoka taasisi ya ALIMA ambayo ndio inasimamia kituo hiki anasema…

 Tulichunguza damu ya mtoto, tukachukua sampuli kutoka kwa mama mzazi na pia tukapima majimaji ya mfuko wa uzazi, tukihofu pengine kuna virusi. Baada ya uchunguzi wa kina majibu yalionesha hakuna virusi. Hii ndio sababu hata sisi wenyewe tunastajabu na kushangaa kwa mtazamo wa kisayansi.”

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload