Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Simulizi ya filamu The Proposal-2009

January 11, 2019

The Proposal ni filamu ya kuchekesha iliyotolewa 2009, iliyoongozwa na Anne Fletcher na kuigizwa na Sandra Bullock na Ryan Reynolds.

Filamu hii ilitungwa na Pete Chiarelli.

 Simulizi ya filamu [The proposal]

 

Margaret Tate ni mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu inayoitwa Ruick & Hunt Publishing. Wafanyikazi wake hawapendi uongozi wake. Baada ya kupata habari kuwa atarudishwa kwao nchini Canada, yeye anamlazimisha mtumishi wake, Andrew Paxton, amuowe ili apate kubaki nchini Marekani. Andrew anakubali kumuowa Margaret, lakini kwa masharti.

Wawili hawa wanaenda likizo kwa wazazi wa Andrew, kijijini Sitka, Alaska ili kuwadangaya familia yao kuwa wanaowana.

 

Margaret anashikwa na bumbuwazi pindi anapogundua kuwa familia ya kina Andrew ni matajiri wanaomiliki biashara nyingi kijijini Sitka. Baada ya sherehe iliyoandaliwa nyumbani, Andrew anatangaza kuwa atamuowa Margaret.

 

 

Familia ya Andrew ilipokea habari hizo kwa furaha (isipokuwa babake Andrew) na wanapanga kuwa harusi ifanywe wiki hiyo hiyo. Harusi inapofanyika Margaret anaamua kuwa hawezi kuolewa na Andrew, na anatubia mbele ya kila mtu kuwa hiyo ilikuwa harusi ya uwongo.

 

Margaret anaarifiwa kuwa ana saa 24 za kurudi Canada. Kwa sababu Margaret alikubali hatia aliyofanya, Andrew hakupelekwa jela. Margaret alirudi New York, na kufunganya vitu vyake.

 

Andrew anakimbilia kumfuata na anampata Margaret ofisini anapomuambia kuwa anampenda mbele ya watu wote ofisini. Andrew anamposa Margaret, na wawili hawa  wanakuwa  wachumba, na mara hii inakuwa "kikwelikweli"

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload