Ujenzi wa Lambo la Aswan nchini Misri unaanza-1960


Tar

Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani.

Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake

Lambo la Aswan iko katika Misri ya Kusini kwenye mto Nile. Ukuta wake uko kilomita 13 kusini ya mji wa Aswan.

Hapa maji ya Nile yazuiliwa na kuwa ziwa la Nasser linaloelekea hadi ndani ya Sudani.

Lambo lilijengwa kuanzia tarehe 9 januari mwaka 1960, Shabaha yake kuu ni kuzuia mafuriko ya mto Nile yaliyohatarisha maisha ya watu kanda ya mto.

Tatizo lake kubwa ni ya kwamba lilivurugisha ekolojia ya mto.

Mafuriko yalileta pia matope yenye rutuba yanayobaki ziwani na kujaza polepole ziwa lenyewe.

Maji mengi hupotea kila siku kwa njia ya uvukizaji kwa sababu uso wa ziwa uko katika nchi yenye joto kali.

Shabaha ya kujenga lambo

Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.

lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.

Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili ziko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.

Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.

Shida za malambo

1.Ukuta unaathiri uwiano wa ekolojia; kwa mfano lambo la Aswan linazuia matope yenye rutuba yasifikie Misri

2. Umwagiliaji katika nchi za joto unaweza kuharibu ardhi ukiiongezea chumvi kwa njia ya uvukizaji

3.Mara nyingi wenyeji wamefukuzwa katika eneo la ziwa jipya bila kupewa makazi mazuri

4.Penye hatari ya tetemeko la ardhi uzani wa maji umeongeza matetemeko

5. Lambo linaweza kusababisha ajali na hata maafa likipasuka na kiasi kikubwa cha maji kilichozuiliwa na ukuta wake kushuka ghafla na kuharibu makazi ya watu, mashamba na miundombinu kwenye njia yake.​

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu