Jumba la maonyesho linalovutia mamilioni ya wageni wanaodhuru mjini Paris Ufaransa


Louvre ni jumba la maonyesho la mjini Paris, Ufaransa, ambalo linavutia mamilioni ya wageni wanaodhuru hapo kwa sababu ya mkusanyiko wa sanaa zilizojaa katika jumba hilo.

Kiasili Louvre ilikuwa jumba la wafalme wa Ufaransa katika mji wa Paris

Tangu uhamisho wa mfalme Louis XIV alijenga jumba jipya huko Versailles ilikaa tu ikatumiwa kwa shughuli mablimbali za kupokea kazi za sanaa.

Tangu mapinduzi ya Ufaransa ilifunguliwa kwa watu wote. Maonyesho ya sanaa yaliendelea kupanushwa na kuboreshwa leo hii Louvre ni makumbusho na maonyesho ya sanaa duniani inayotembelewa na watu wengi kila mwaka.

Picha iliyomaarufu kabisa katika jengo la Louvre ni ile ya Mona Lisa iliyochorwa na Leonardo da Vinci, lakini pia kuna michoro ya wasanii wengine kama vile Renoir, Rembrandt, Rubens, na Titian.

Piramidi mpya katika uwanja wa jumbaa ilijengwa na I. M. Pei.

Pia kuna sanamu za kuchonga katika jengo hilo la Louvre. Masanamu yaliyomaarufu katika jengo hilo ni pamoja na la Venus de Milo na Nike wa Samotraki.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu