Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.01.2019: Philippe Coutinho, Barella, Suarez, Dybala, Cesc Fabregas

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemshauri Fabregas kuihama klabu hiyo ya Stamford Bridge kwa maslahi ya uchezaji wake.

Uhamisho wa Cesc Fabregas kwenda Monaco unakwamishwa na hali kwamba klabu hiyo ya Ligue 1 bado haijaafikiana na klabu ya Chelsea kuhusu ada ya uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 31.

Manchester United wameanzisha mazungumzo na Barcelona wakitaka kumsajili mshambuliaji Mbrazil Philippe Coutinho, 26, lakini ndipo waweze kumnasa itabidi wachomoe zaidi ya £100m.

Juventus wanasema wanaweza wakashawishika kumuuza Paulo Dybala, 25, ambaye anatafutwa na Manchester City mwisho wa msimu, lakini mradi tu ada ya uhamisho wa raia huyo wa Argentina iwe zaidi ya £90m.

Manchester City, Bayern Munich na Paris St-Germain wote wamewasilisha ofa kumtaka Dybala lakini zikakataliwa.

Chelsea wanamnyatia kiungo wa kati wa Cagliari Nicolo Barella ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m,

lakini huenda wakakumbana na ushindani kutoka kwa Napoli na Inter Milan ambao pia wanataka saini ya kijana huyo wa miaka 21. Mchezaji huyo hata hivyo anadaiwa kutotaka kuihama klabu hiyo ya Serie A wakati wa dirisha la sasa la uhamisho wa wachezaji.

Unai Emery amewahimiza Arsenal kutafuta pesa za kukamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 25, mwezi huu.

Klabu hiyo ya Uhispania inadaiwa kuwa tayari kumwachilia mchezaji huyo kwa mkopo iwapo kutakuwa na ahadi ya kutoa £20m kumchukua Suarez kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu