Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Hatua zaidi zinahitajika kukabiliana na usafirishaji haramu kwenye mizozo-UNODC

January 8, 2019

Tokomeza usafirishaji wa binadamu. Kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya UNODC asilimia 30 ya watu wanaosafirishwa kiharamu ni watoto.

kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za kimataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu iliyozinduliwa  mjini Vienna, Austria inasema  kuwa Idadi ya waathirika wa usafirishaji haramu imeongezeka, huku idadi ya makundi yaliyojihami na magaidi wanawasafirisha wanawake na watoto kwa ajili ya kupata fedha na kuwaandikisha kama wafuasi,

Akiwasilisha ripoti hiyo ambayo imetathmini nchi 142 kuhusu mienendo ya usafirishaji haramu na uhalifu huo katika maeneo ya mizozo ya silaha,

 mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambamba na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC , Yury Fedeotov amesema,

 

“watoto wanaotumikishwa jeshini, kazi ya lazima utumikishwaji kingono, usafirishwaji haramu umechukua sura mpya ya kusikitisha wakati vikundi vilivyojihami na magaidi wakisambaza hofu na kutumia vishawishi ili kuwapata wafuasi wapya.

 Bwana Fedotov amesema ripoti imeonesha wazi kuwa kuna haja ya kuimarisha ufadhili wa kiufundi na ushrikiano, kusaidia nchi kulinda manusura wake na kuwawajibisha wahalifu mbele ya sheria ili kufikia malengo ya maendeleo

endelevu, SDGs.

  kwa mujibu wa ripoti.  imebaini kuwa kuna ongezeko la watoto wanaosafirishwa ikiwa ni asilimia 30 ya visa vyote huku wasichana wengi wakiathirika zaidi ikilinganishwa na wavulana. Ukatili wa kingono ndio kichocheo kikubwa cha usafirishaji haramu ikijumuisha asilimia 59 ya visa vyote.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload