Mwanaharakati aliyepiga vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, miaka ya 1960's


Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi, baadae akaanzisha vuguvugu la Black Consciouness Movement (Harakati za kujitambua kwa watu weusi).

Vuguvugu hili lilipata nguvu sana na kuenea karibuni katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.

Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni na kuteswa na maaskari wa serikali ya kibaguzi.

Biko alijulikana kama jabali la harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi. Wakati yupo hai, alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za kujaribu kuwatia nguvu watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake wa kusema kwamba "black is beautiful" akimaanisha kwamba "mtu mweusi ni mzuri."

Alielezea maana ya msemo huu ni: "mtu, ni sawa kama ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu