Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 07.01.2019: Denis Suarez, Tammy Abraham, Manolas, Under, Foden, Maja, Kostas Manolas

January 7, 2019

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu beki wa AS Roma kutoka Ugiriki Kostas Manolas, 27, ambaye ana kifungu cha £32m cha kumfungua kutoka kwenye mkataba wake.

Kostas Manolas,

 

Arsenal hawatarajiwi kutoa ofa nyingine kumtaka winga wa AS Roma Cengiz Under ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m baada ya ofa yao ya awali ya £35m ya kumtaka mchezaji huyo wa Uturuki mwenye miaka 21 kukataliwa

Cengiz Under

 

Barcelona wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hawamuuzi kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez, 25, kwa Arsenal mwezi huu.

Denis Suarez

 

Wolves wamekamilisha mpango wa kumchukua Tammy Abraham kutoka kwa klabu yake ya Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Tammy Abraham

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 21 anatarajiwa sasa kufanya uamuzi leo Jumatatu kuhusu iwpao atakatisha mkopo wake Aston Villa na kwenda Molineux.

 Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba haiwezekani kwa winga raia wa England Phil Foden mwenye miaka 18 kuondoka klabu hiyo kwa mkopo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon