Je wajua jengo mashuhuri duniani ambalo ni kielelezo cha sanaa na usanifu wa Ugiriki ya Kale.


Uso wa mashariki wa Parthenon

Parthenon ni hekalu kwenye Akropolis mjini Athens iliyojengwa wakati wa Ugiriki ya Kale. Ni kati ya majengo mashuhuri duniani na kielelezo cha sanaa na usanifu wa Ugiriki ya Kale

Parthenon Ilikuwa hekalu ya mungu wa kike Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu mlinzi wa mji wa Athens ya kale.

Hekalu ilijengwa katika karne ya 5 KK baada ya ushindi wa Wagiriki juu ya Waajemi. Wagiriki waliamini ya kwamba mungu Pallas Athena aliwaokoa. Baadaye serikali ya Athens ilitumia kama jengo la kutunza hazina ya dola.

Baada ya uenezaji wa Ukristo hekalu iligeuzwa kuwa kanisa katika karne ya 6 KK. Baada ya Waosmani kutawala Ugiriki waliitumia kama ghala la baruti kwa jeshi lao

Katika vita kati ya jamhuri ya Venesia na Milki ya Osmani ilipelekea kutokea kwa mlipuko uliovunja sehemu ya jengo la Parthenon

Sehemu za mapambo ya nje ambayo ni uchongaji wa mawe zilipelekwa Uingereza mwaka 1807 na zinaonyeshwa katika makumbusho ya Britania mjini London.

Jengo linaloiga Parthenon mjini Nashville,Marekani

Serikali ya Ugiriki inadai kurudishwa kwa sehemu hizo

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu