ILO yaleta ahueni kwa wakulima wa tangawizi Myanmar


Shirika la kazi duniani, ILO limechukua hatua kusaidia wakulima wa zao la tangawizi nchini Myanmar ambao wamekuwa wakiathirika kiafya kutokana na kilimo cha zao hilo.

Katika jimbo la Shan nchini Myanmar barani Asia, zao la tangawizi linawakilisha njia muhimu ya maisha kwa mamia ya wakulima.

Hata hivyo wamekuwa wakiathirika kiafya siyo tu kwa sababu ya kufanya kazi kwa saa nyingi chini ya jua kali, bali pia kemikali zinazotumika katika kilimo hicho.

Uba Loon mmoja wa wakulima anasema kilimo cha tangawizi kinahusisha kazi ngumu ya kulima siku nzima juani na kunyanyua mizigo mizito wakati wa kuvuna lakini hatari zaidi iko kwenye dawa za kuua wadudu

Ili kupambana na hali hiyo, shirika la kazi kazi duniani ILO kupitia mradi wake wa Vision Zero Fund linawapatia wakulima taarifa na elimu ya matumizi bora ya kemikali za kilimo.

Chini ya mradi huo wakulima wa tangawizi wanafundishwa kuhusu usalama wa afya ili kupunguza hatari zinazotokana na uzalishaji wa zao hilo.

Mariana Infante Villarroel, mshauri mkuu katika mradi huo wa ILO nchini Mynmar anasema,

“Tunawafundisha kuhusu usalama na afya na mambo kadha kuhusu jinsi ya kudhibiti wadudu kisha mwisho wanasema mambo ambayo yanaendana na jamii yao”

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu