Je wajua jengo mashuhuri duniani ambalo ni kielelezo cha sanaa na usanifu wa Ugiriki ya Kale.

January 6, 2019

Uso wa mashariki wa Parthenon

 

Parthenon ni hekalu kwenye Akropolis mjini Athens iliyojengwa wakati wa Ugiriki ya Kale. Ni kati ya majengo mashuhuri duniani na kielelezo cha  sanaa na usanifu wa Ugiriki ya Kale

 Parthenon Ilikuwa hekalu ya mungu wa kike Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu mlinzi wa mji wa Athens ya kale.

Hekalu ilijengwa katika karne ya 5 KK baada ya ushindi wa Wagiriki juu ya Waajemi. Wagiriki waliamini ya kwamba mungu Pallas Athena aliwaokoa. Baadaye serikali ya Athens ilitumia kama jengo la kutunza hazina ya dola.

 Baada ya uenezaji wa Ukristo hekalu iligeuzwa kuwa kanisa katika karne ya 6 KK. Baada ya Waosmani kutawala Ugiriki waliitumia kama ghala la baruti kwa jeshi lao

Katika vita kati ya jamhuri ya Venesia na Milki ya Osmani  ilipelekea kutokea kwa  mlipuko  uliovunja sehemu ya jengo la  Parthenon

Sehemu za mapambo ya nje ambayo ni uchongaji wa mawe zilipelekwa Uingereza mwaka 1807 na zinaonyeshwa katika makumbusho ya Britania mjini London.

Jengo linaloiga Parthenon mjini Nashville,Marekani

 

Serikali ya Ugiriki inadai kurudishwa kwa sehemu hizo

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon