Papa Leo X anamtenga padri Martin Luther na Kanisa Katoliki-1521


Tarehe 3 Januari mwaka 1521 Papa Leo X anamtenga Padri Martin Luther na Kanisa Katoliki.

Papa Leo X (Alizaliwa tarehe 11 Desemba 1475 – na kufariki tarehe 1 Desemba 1521)

alikuwa papa kuanzia tarehe 9 Machi 1513 hadi kifo chake.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giovanni di Lorenzo de' Medici.

Alimfuata Papa Julius II akafuatwa na Papa Adrian VI.

Leo X ndiye aliyemtenga Martin Luther na Kanisa Katoliki tarehe 3 Januari 1521.

Martin Luther akiwa na umri wa miaka 46

Martin Luther (alizaliwa Tarehe 10 Novemba 1483 – na kufariki Tarehe 18 Februari 1546) alikuwa Mkristo mwanateolojia kutoka nchi ya Ujerumani maarufu kama mwanzilishi wa Uprotestanti.

Kisha kushindana na Papa wa Roma, na kutengwa na Kanisa Katoliki, aliongoza Matengenezo ya Kiprotestanti yaliyosababisha mapema madhehebu mengi mapya kutokana na wazo kuu la kwamba Biblia inajitegemea na kumtosha kila anayesoma.

Aliandika vitabu vingi, kutunga nyimbo kadhaa na hasa kutoa tafsiri maarufu ya Biblia ya Kikristo katika lugha ya Kijerumani.

Athari yake imekuwa kubwa sana katika Kanisa na ulimwengu kwa jumla.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu