Murder Was the Case [Snoop Doggy Dogg]

Murder Was the Case ni jina la filamu na albamu ya kibwagizo kifupi cha mwaka wa 1994 ambacho kimechezwa na Snoop Doggy Dogg

Filamu hii yenye urefu wa dakika 18 iliongozwa na Dr. Dre na Fab Five Freddy ikiwa na hadithi ya kifo cha Snoop Dogg na kufufuka kwake baada ya kuingia mkataba na Shetani.

Jina la filamu linatokana na wimbo wa Snoop ambao upo katika albamu yake ya kwanza, Doggystyle, ambao ulitoka mapema kabla ya filamu hii.

Albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 mnamo Novemba 5, 1994 ikiwa na mauzo yapatayo 329,000 katika wiki yake ya kwanza na vilevile ilipata kutamba katika chati za albamu Top R&B/Hip-Hop.

Wiki iliyofuata ilikaa nafasi ya juu ikiwa imeuza nakala 197,000 na kupewa hadhi ya Dhahabu. Albamu ilitunukiwa hadhi ya platinum 2x ikiwa na mauzo ya nakala 2,030,000.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu