Alianzisha kundi la kidini la wanahisabati waliotafuta siri za dunia katika namba-Pythagoras

Alikataa kuua wanyama kwa sababu aliona roho ndani ya wanyama pia, hivyo wanafunzi wake nao hawakula nyama.

Pythagoras alikuwa mtaalamu wa falsafa na hisabati wakati wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale.

Pythagorasi alianzisha kundi la kidini la wanahisabati; walitafuta siri za dunia katika namba wakiamini ya kwamba miungu walificha habari za dunia ndani ya namba zinazoonekana kote duniani kwa wataalamu wa hisabati.

Pythagoras anakumbukwa hasa kwa "uhakiki wa Pythagoras" unaoeleza tabia za pembetatu mraba. Aligundua ya kwamba mraba juu ya hipotenusi (kiegana au upande kinyume cha pembe mraba) ni sawa na jumla ya miraba juu ya pande mbilinyingine

Wanafunzi wake walifundisha uhamisho wa roho za watu kutoka mwili mmoja kwenda mwili mwingine; miili hufa.lakini roho za dumu. Pythagorasi alidai ya kwamba yeye alikumbuka maisha yake manne ya awali.

Alizaliwa kisiwani Samos karibu na pwani ya Asia Ndogo.

Alipokuwa na umri wa miaka 14 alihamia Italia ya kusini iliyokuwa eneo lenye miji mingi ya Wagiriki wa Kale.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu