Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 03.01.2019: Eriksen, Ramsey, Abraham, Ozil, Doucoure na Defoe.

January 3, 2019

Wolves wamewasilisha ofa ya £18m kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa inayocheza ligi ya Championship

Tammy Abraham

 

Christian Eriksen anagoma kutia saini mkataba mpya Tottenham, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye miaka 26 ukitarajiwa kufikia kikomo baada ya miezi 18.

Christian Eriksen

 

Juventus wamethibitisha kwamba wameonyesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, bila kulipa ada yoyote baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu. 

Aaron Ramsey, 28

 

Bournemouth watamruhusu mshambuliaji wa England Jermain Defoe kuondoka klabu hiyo Januari. Mchezaji huyo wa miaka 36 amechezeshwa mara nne pekee kama nguvu mpya ligini msimu huu.

Jermain Defoe

 

Mesut Ozil, 30, amesisitiza kwamba mustakabali wake bado upo Arsenal licha ya kutafutwa na Real Madrid na Inter Milan.

Mesut Ozil

 

Watford hawataki kumuuza Abdoulaye Doucoure, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £50m kwa Paris St-Germain wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji la Januari

 www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon