Je wamjua Mwanafalsa aliyekataa dini na imani ya Mungu katika maisha yake.

Karl Marx alikuwa mwanafalsafa kutoka nchini Ujerumani ambaye pamoja na Friedrich Engels alianzisha siasa ya ukomunisti.

Baada ya kuhamia Brussels katika Ubelgiji alitunga pamoja na Engels kijitabu cha Manifesto ya Chama cha Kikomunisti (Ilani ya kikomunisti) alimotangaza imani yake ya kwamba

"historia ya jamii zote ni historia ya mapambano ya matabaka''

Kwa Karl Marx kazi ya falsafa haikuwa kueleza dunia ilivyo bali kuibadilisha.

Alifundisha ya kwamba mawazo, fikra na imani zote zinatokana na hali ya uchumi na teknolojia katika jamii

aliona historia haisukumwi na "roho ya ulimwengu" bali na nguvu za uchumi wa jamii na namna ya kujipatia riziki za maisha

Kutokana na msingi huu Marx alikataa dini na imani ya Mungu. Kwake dini ni itikadi ya jamii ya uwongo na pamoja na sahihisho la jamii alitarajia ya kwamba dini itapotea.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu