Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Kwanini Januari ndio mwezi wa kwanza wa mwaka

January 2, 2019

Jinsi ilivyoamuliwa kwamba Januari ndio mwezi wa kwanza wa mwaka

 Kila mwaka tarahe kama hii watu kutoka kote duniani hukaribisha mwaka mpya kwa fataki, kupiga filimbi, pamoja na vinywaji.

 

Lakini kabla ya kuanza sherehe hizo uliwahi kufikiria ni kwa nini tarehe mosi Januari ndio inayoadhimishwa kuanza kwa mwaka mpya?

 

Kila kitu kinatokana na mila na tamasha za Roma, na kalenda iliozinduliwa na Julius Caesar miaka 2000 iliopita.

 Lakini pia huwezi kumwacha nje papa aliyejulikana kwa jina Gregorio wa kumi na tatu

Kwa Waroma wa zamani .Januari ilikuwa muhimu kwa sababu ulikuwa mwezi uliotakaswa kwa mungu Janus [hivyobasi ukaitwa Ianuarius, ikimaanisha Januari kwa kilatino.]

"Inahusishwa na kuangalia mbele na nyuma," anaelezea Diana Spencer, profesa katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza

 

Kwa hiyo ikiwa kuna muda katika mwaka ambao unapaswa kuamua, huu ndiyo wakati tunapoanza tena." Ni mantiki kuwa hivi ''

 

Pia unafanana na muda kama ule wa Ulaya ambapo siku zinaanza kuwa ndefu baada ya msimu wa baridi.

 

"Waroma walihusishwa nao sana kwa sababu hutokea baada ya siku fupi, wakati ambapo dunia ina giza ,baridi na hakuna kitu kinachomea, kulingana na Professa Spencer.

 

Ni Muda wa kupumua na kutafakari''.

 

Baada ya Waroma kuwa na mamlaka zaidi, walianza kusamabaza kalenda yao katika ufalme wao mkubwa.

Kulingana na itikadi za Roma, Janus ni mungu wa nyuso mbili, mwanzo na mwisho

 

Lakini katika miaka ya kati , baada ya kuanguka kwa ufalme wa Roma , Ukristo ulikuwa umejiimarisha hivyobasi tarehe mosi januari ilionekana kuwa tarehe ya Kipagani.

 Mataifa mengi yaliotawaliwa na Ukristo walitaka mwaka mpya kuadhimishwa tarehe 25, ambayo inaadhimisha tarehe ambayo malaika Jibreel alijitokeza kwa bikra Mariam mtakatifu.

 ''Ijapokuwa siku ya krisimasi ni siku ya kuzaliwa kwa Yesu, tarehe muhimu ni wakati malaika huyo alipomwambia Mariam kwamba atajifungua mwana'', 

 

Huo ndio wakati ambapo hadithi ya Yesu ilianza , hivyobasi ilikuwa na maana kuu kutaka mwaka mpya kuanza siku hiyo.

 

Papa Gregorio wa 13 alishinikiza mwanzo wa mwaka kuwa mwezi Januari badala ya mwezi Machi

 

hatahivyo Uingereza ambayo ilipinga amri ya papa na kuchukua dini ya Wapinzani wa papa waliendelea kusherehekea Machi 25 hadi mwaka 1752.

 

Mwaka huo sheria ya bunge la Uingereza ilioana na ile ya mataifa menbgine ya Ulaya.

 Leo, mataifa mengi huongozwa na kalenda hiyo ya Gregorian, na ndio sababu fataki hupigwa kote duniani ifikiapo tarehe mosi mwezi januari kila mwaka.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload