Je wamjua Mwanafalsa aliyekataa dini na imani ya Mungu katika maisha yake.

January 2, 2019

Karl Marx  alikuwa mwanafalsafa kutoka nchini Ujerumani ambaye pamoja na Friedrich Engels alianzisha siasa ya ukomunisti.

Baada ya kuhamia Brussels katika Ubelgiji alitunga pamoja na Engels kijitabu cha Manifesto ya Chama cha Kikomunisti (Ilani ya kikomunisti) alimotangaza imani yake ya kwamba

"historia ya jamii zote ni historia ya mapambano ya matabaka''

Kwa Karl Marx kazi ya falsafa haikuwa kueleza dunia ilivyo bali kuibadilisha.

Alifundisha ya kwamba mawazo, fikra na imani zote zinatokana na hali ya uchumi na teknolojia katika jamii

 aliona historia haisukumwi na "roho ya ulimwengu" bali na nguvu za uchumi wa jamii na namna ya kujipatia riziki za maisha

 Kutokana na msingi huu Marx alikataa dini na imani ya Mungu. Kwake dini ni itikadi ya jamii ya uwongo na pamoja na sahihisho la jamii alitarajia ya kwamba dini itapotea.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon