Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 01.01.2019: Ozil, Ramsey, Pogba, Hudson-Odoi, Rabiot

Kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil, 30, amesema hataihama klabu yake ya Arsenal kwa mkopo mwezi huu wa Januari. Badala yake, amesema yuko tayari kusalia kupigania nafasi yake katika kikosi.

Juventus wamewasilisha ofa kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 28, ambapo wanataka kumpa mkataba wa miaka minne ambapo atakuwa analipwa £138,000 kila wiki.

Wales Aaron Ramsey,

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anawakosea heshima wapinzani wake kwa jinsi anavyosherehekea kufunga mabao,

hilo ni kwa mujibu wa kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Claude Makelele.

anasema Pogba amekuwa akisherehekea kufunga mabao kwa kucheza ngoma,

lakini Makelele anaamini amevuka mipaka. "Inaudhi sana. Namshauri Pogba. Nataka kumwambia, 'Sikiliza, fanya hivyo ukiwa katika chumba cha kubadilishia mavazi, sio [uwanjani]. Inaudhi sana. Mnashinda 4-0, kisha unacheza ngoma hapa mbele yangu," amesema Makelele

Claude Makelele.

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot hana mpango wowote wa kuhamia Tottenham kwa sababu anaichukulia klabu hiyo kuwa ya chini ya kiwango chake kama mchezaji. Mchezaji huyo wa miaka 23 hata hivyo bado anataka kuihama

Mwenyekiti na mmiliki wa Huddersfield Dean Hoyle hana nia ya kuiacha klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England iendeleze kuteleza na kushushwa daraja na ameahidi kuwanunua wachezaji zaidi Januari

Chelsea wamekataa ofa ya zaidi ya £20m kutoka kwa Bayern Munich wanaomtaka winga wa England anayechezea timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 19 Callum Hudson-Odoi, 18.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu