Eneo la mfereji wa Panama linarudishwa kwa serikali ya Panama kutoka kwa utawala wa Marekani--1999

[Tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka 1999 utawala wa Marekani unarudisha mfereji wa Panama kwa serikali ya Panama]

Mfereji wa Panama ni njia ya maji nchini Panama (Amerika ya Kati) kati ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Atlantiki.

Shingo ya nchi ya Panama ni njia fupi kati ya bahari zote mbili

Mfereji wa Panama

Kabla ya kujengwa kwa mfereji huu meli zote zilipaswa kuvuka ncha ya kusini ya Amerika na mfereji umefupisha safari hii kwa kilomita nyingi sana.

Utangulizi wa mfereji ulikuwa reli kutoka Colon upande wa Karibi kwenda mji wa Panama upande wa Pasifiki iliyojengwa 1855.

Reli hii ilirahisisha safari kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na bidhaa na ilipelekea watu kwenda Kalifornia.

Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya dhahabu iliyopatikana kule tangu 1848 na hapakuwa na reli kati ya pwani zote mbili za Marekani wakati ule.

Kampuni ya Kifaransa ilianza kujenga mfereji tangu 1880 lakini ilishindwa. Serikali ya Marekani iliendeleza kazi na kumaliza mfereji mwaka 1914.

Marekani ilitawala kanda ya mfereji kuanzia 1904 hadi mwaka 1999 kwa kuikodi kutoka nchi ya Panama.

Siku hizi mfereji uko chini ya serikali ya Panama.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu