Muasisi wa TANU na moja kati ya wapigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950

Ally Kleist Sykes (alizaliwa Gerezani, Dar es Salaam, tarehe 10 Oktoba 1926 - na kufariki Nairobi, Kenya, mnamo tarehe 19 Mei 2013)

Ally Sykes na Mwalimu Julius Nyerere 1958

alikuwa mzalendo muasisi wa TANU na moja kati ya wapigania uhuru wakubwa wa Tanganyika katika miaka ya 1950

Ally Sykes ndiye aliyemwandikia na Kumkabidhi Mwalimu Julius Nyerere kadi ya TANU Na. 1.

Ally Sykes mmoja wa waasisi wa TANU, mmoja wa wale watu wasiozidi takriban saba walikuwa katika kamati ya ndani ya TAA iliyounda TANU,

mmoja wa wafadhili wakuu wa TANU, mmoja wa askari kwa maana yake halisi kwa kuwa ni Ally Syke ndiye TAA hadi TANU ikimtegemea kwa kutekeleza mambo ya hatari dhidi ya Waingereza.

Ally Sykes ndiye alikuwa akipewa kazi za hatari za kumwaga ‘’sumu na upupu’’ dhidi ya serikali.

Sumu na upupu yalikuwa makaratasi aliyokuwa akichapa nyumbani kwake usiku makaratasi ambayo Waingereza waliyaita makaratasi ya ‘’uchochezi.’’

Waingereza na makachero wake walikuwa wanamjua Ally Sykes vizuri. Waingereza walikuwa wakijua kuwa alikuwa na medali ya mlenga shabaha bingwa aliyopata Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Abdulwaid na Ally Sykes wakiwa 6th Battalion Burma Infantry King's African Rifles (KAR) Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945)

Huyu ndiye Ally Sykes mzalendo muasisi wa TANU ambaye sahihi yake ndiyo iko katika kadi ya TANU ya Baba wa Taifa.

Ally Kleist Sykes na Peter Horace Colmore, mjini Paris 1963

Ally Sykes alikuwa mtu maarufu kupita kiasi. Alikuwa kwanza ana umaarufu wa kuzaliwa. Kazaliwa Dar es Salaam Gerezani, mtoto wa mjini. Kisha alikuwa maarufu kwa nasaba.

Baba yake Kleist Sykes alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika siasa zote za Dar es Salaam katika miaka ya ya mwanzo ya 1900 hadi alipofariki mwaka 1949.

Baba yake alikuwa maarufu kwa kuwa alilelewa na Afande Plantan askari kiongozi katika jeshi la Wajerumani lilokuja Tanganyika na Herman Von Wissman wakati Wajerumani walipoingia kuitawala Tanganyika

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu