Texas inajiunga na Marekani kama jimbo la 28 Mwaka 1845

December 29, 2018

 [Tarehe 29 mwezi wa 12 mwaka 1845 Texas inajiunga  na Marekani na kuwa jimbo la 28]

 

Texas ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Idadi ya wakazi wa jimbo lote hufikia watu 24,326,974 (2008) wanaokalia eneo la 696,241 km² ambalo ni hasa milima na jangwa

Upande wa mashariki ni maji ya ghuba ya Mexico. Mji mkuu wa jimbo ni Austin na mji mkubwa jimboni ni Houston. Imepakana na Oklahoma, Arkansas, Louisiana, New Mexico (Meksiko Mpya) na nchi ya Meksiko (Chihuahua, Coahuila, Nuevo León na Tamaulipas).

Kabla ya kufika  kwa  Wahispania, maeneo ya Texas yalikaliwa na makabila mbalimbali ya Waindio. Tangu uvamizi wa Mexiko wa Waazteki kulikuwa na misafara kadhaa ya Wahispania kwenye pwani la Texas lakini hawakukaa.

 Baada ya Ufaransa kuanzisha koloni la Lousiana katika eneo la New Orleans Hispania iliogopa uenezaji wa Wafaransa, wakapeleka mapadre Mexiko waliojenga misioni kadhaa huko.

 na mwaka 1718 mji wa San Antonio ulianzishwa. Lakini idadi ya walowezi Wahispania ilikuwa ndogo kutokana na upinzani mkali wa Waindio wenyeji.

 

KUJIUNGA KWA TEXAS MAREKANI NA KUWA JIMBO LA 28

 

Nchi hii mpya ilikuwa dhaifu na wakazi wengi waliogopa kuvamiwa upya na Mexiko. Kwa hiyo viongozi waliomba kuingizwa katika Marekani.

 Ilhali Texas ilikuwa na sheria ya utumwa na ndani ya Marekani majimbo ya kukubali na kukataa utumwa yalivutana kwa miaka kadhaa hapakuwa na azimio kuhusu ombi la Texas.

 Maana majimbo yaliyopinga utumwa hayakutaka kuongeza maeneo yenye  utumwa ndani ya Marekani.

 

Lakini mwaka 1845 raisi mpya James K. Polk alitangaza utekaji wa Texas, na Texas ikawa jimbo la 28 katika Maungano ya Madola ya Amerika.

 Hatua hii ilisababisha vita ya Marekani na Mexiko vilivyomalizika baada ya miaka miwili kwa ushindi wa Marekani mwaka 1848

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon