Kim Jong-un awa kingozi mkuu wa Korea Kaskazini baada ya mazishi ya baba yake-2011

December 28, 2018

 [Tarehe 28 mwezi wa 12  mwaka 2011 Kim Jong-un  awa kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini].

 

Kim Jong-un  alizaliwa 8 Januari 1982-84 au 5 Julai 1984), ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea (WPK) na kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini.

Kim ni mtoto wa pili wa Kim Jong-il (1941-2011) na Ko Yong-hui. Kabla ya kuchukua madaraka, Kim alikuwa haonekani mara kwa mara kwa umma. Maelezo kama vile mwaka gani alizaliwa, na kama alienda kweli shule nchini Uswisi akitumia jina la uongo, ni vigumu kuthibitisha.

Mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini lakini Vita baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili.

Kila moja alianzisha serikali yake kulingana na itikadi yake.

 

Warusi waliunga mkono utawala wa Kikomunisti Korea Kaskazini na Wamarekani waliunga mkono uchumi wa kibepari na serikali iliyochaguliwa kwa kura ya wengi Korea Kusini.

 Kim alitangazwa kuwa kiongozi mkuu baada ya mazishi ya baba yake tarehe 28 Desemba 2011. Vyeo vyake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, Mwenyekiti wa Tume ya Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea, na mwanachama wa Kamati ya Kudumu ya Politburo ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea 

Mnamo tarehe 9 Machi 2014, Kim Jong-un alichaguliwa bila kupingwa kuingia katika Bunge Kuu la Watu.

 

 Kim ana shahada mbili, moja ya fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Kim Il-sung, na nyigine kama afisa wa Jeshi katika Chuo Kikuu cha Jeshi cha Kim Il-sung

 Mnamo tarehe 12 Desemba 2013, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilitangaza kwamba kwa sababu ya "udanganyifu," aliamuru mauaji ya mjomba wake Jang Song-thaek.

 Kim Jong-un anaaminika kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya kaka yake wa kambo, Kim Jong-nam nchini Malaysia mwezi Februari 2017.

 

www.mzunguko.com

 


 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon