Ghasia zaibuka mjini Mombasa baada ya Mwai kibaki kujitangaza mshindi wa Uchaguzi wa Rais mwaka 2

[Tarehe 27 mwezi wa 12 mwaka 2007 machafuko yaibuka Mombasa na maeneo mengine nchini kenya Baada ya Mwai kibaki kujitangaza mshindi wa Urais wa mwaka 2007]

Mwai Kibaki ni rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya,Mzee Jomo Kenyatta, na Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley.

Uchaguzi wa urais 2007

Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais.

Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,ODM , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya.

Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu;

baada ya kuendelea na matangazo Kibaki alionekana kuwa mbele.

Kulikuwa na hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa yakiegemea upande wake kwa kumwongezea kura.

Hisia hizi zilisababisha ghasia kuibuka Nairobi,kisumu,Eldoret,kericho na Mombasa na sehemu zingine nchini Kenya.

Hatahivyo Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi;

hafla ilifanywa katika Bustani ya Ikulu ya Nairobi mbele ya waalikwa wachache walioruhusiwa kushuhudia.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu