Kuundwa kwa IMF (Shirika la Kimataifa la Fedha)-1945

December 27, 2018

[Tarehe 27 mwezi wa 12 mwaka 1945 Shirika la Kimataifa la Fedha linaundwa]

Shirika la Fedha Duniani (IMF) linajumuisha nchi 189; na lengo lake kuu ni kuleta utulivu wa kifedha duniani.

Kazi kubwa ya Shirika la IMF ni kuzisaidia nchi zinazokabiliana na hatari ya kufilisika. Makao yake makuu yapo mjini Washington, Marekani.

Christine Lagarde

 

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hili kwa sasa ni Christine Lagarde, waziri wa fedha wa zamani wa Ufaransa.

 Jengo la makao makuu ya IMF mjini Washington DC.

 

IMF (kifupisho cha International Monetary Fund) ni Shirika la Fedha la Kimataifa. Lilianzishwa mwaka 1945 kwa shabaha ya kuboresha ushirikiano katika mambo ya fedha duniani.

 

Kazi yake ni kuangalia siasa ya fedha na benki duniani na kuifanyia utafiti. Inatoa misaada na ushauri ikitakiwa.

 

Si shirika halisi la Umoja wa Mataifa, lakini hushirikiana na UM

 

Nchi tajiri za Ulaya pamoja na Marekani zinaongoza IMF kwa sababu ni nchi zilizoweka pesa zaidi katika mfuko wake. 

 

Mwenyekiti wa IMF huwa anatoka katika nchi za Ulaya na makamu wake ni kutoka Marekani.

 IMF hushirikiana kwa karibu na Benki ya Dunia.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon