Teofilo Hiobo Kisanji alikuwa mwalimu, mchungaji na askofu Mwafrika wa kwanza wa Kanisa la Moravian

[Tarehe 26 mwezi wa 12 mwaka 1915 alizaliwa Teofilo Hiobo Kisanji]

Teofilo Hiobo Kisanji (alizaliwa 26 Desemba 1915 - na kufariki tarehe 15 Aprili 1982) alikuwa mwalimu, mchungaji na baadaye askofu Mwafrika wa kwanza wa Kanisa la Moravian Tanzania

Kisanji alizaliwa katika kijiji cha Chadodwa kwenye wilaya ya Sikonge katika familia ya Wanyamwezi Wakristo.

Baba yake alikuwa mwinjilisti wa kanisa la Moravian. Akasoma ualimu akafundisha shuleni tangu 1933 na baadaye kama mwalimu wa chuo cha ualimu.

1949 akafuata wito wa kuwa mchungaji wa kanisa akibarikiwa 1950. Alisoma theolojia huko Uingereza na Uholanzi akarudi Tanzania kuwa mchungaji Tabora mjini

1962 alichaguliwa kuwa mchungaji kiongozi kwa cheo cha "superintendent" akiwa Mwafrika wa kwanza katika kanisa lake. 1965 akateuliwa kuwa askofu Mwafrika wa kwanza katika kanisa la Moravian Tanzania akasimamia jimbo la Tanzania Magharibi (Tabora). Alikuwa askofu wa Moravian Mwafrika wa pekee nchini Tanzania hadi 1979.

Kisanji alikuwa kati ya viongozi wa makanisa waliojenga umoja wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Mwaka wa 1968 alishiriki katika azimio la kuanzisha chuo cha Motheco mjini Chunya. Aliandika vitabu viwili juu ya historia ya kanisa la Moravian

Aliaga dunia 1982 katika hospitali ya KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre) mjini Moshi akazikwa Tabora.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu