Mvumbuzi wa taa ya solar kwa ajili ya watu wanaoishi mashambani bila umeme.-MKenya

Evans Wadongo (amezaliwa 11 Machi 1986) ni mhandisi kutoka nchini Kenya,

Pia ni mwenyekiti wa chama kisicho cha serikali "Sustainable Development For All-Kenya (SDFA-Kenya)" na mvumbuzi wa taa ya solar kwa ajili ya watu wanaoishi mashambani bila umeme.

Evans Wadongo alizaliwa kama mtoto wa wazazi walimu katika wilaya ya Kakamega, Kenya. Alisoma shule ya msingi Bisunu akaendelea baadaye kwenye sekondari ya Kakamega High School,

alipomaliza akawa miongoni mwa mwanafunzi bora wa Kenya kwa kwa kushika wastani wa A kwenye Kenya Certificate of Secondary Education mwaka 2002.

Akajiunga na Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology akamaliza mwaka 2009 kama bachelor of science

Alipokuwa mwanafunzi mwaka 2004 alivumbua taa ya solar aliyoita "Mwanga Bora" akiwaza matumizi ya nishati ya jua kuwa njia njema ya kuhifadhi mazingira, kupunguza kukatwa kwa miti na kuboresha maisha ya watu mashambani wanaoishi katika mazingira yasiyo na umeme na jinsi ilivyokuwa katika kijiji chake wakati alipokuwa mtoto.

Hakuvumbua taa za solar lakini alitumia teknolojia iliyokuwepo katika nchi zilizoendelea na kuilinganisha na mazingira ya Kenya.

Pamoja na wengine aliunda chama kisicho cha serikali Sustainable Development For All-Kenya (SDFA-Kenya) kilichoendelea kusambaza wazo la kutumia nishati ya jua kwa kuboresha maisha ya watu.

Taa ya solar inatengenzwa kwa bei nafuu na wafundi Wakenya kwa kutumia mabaki ya metali kutoka viwandani na karahana na diodi za LED zinazotumia umeme kidogo.

Mwaka 2010 shirika la habari la CNN ilitambua sifa zake kwa kumpatia cheo cha "shujaa wa CNN" katika la chaguo la "top ten heroes of 2010". Mwaka 2011.

alikabidhiwa tuzo ya mfuko wa Mikhail Gorbachev kwa "watu waliobadilisha dunia"

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu