Nchi ya Libya inapata uhuru kutoka Italia mwaka 1951 na Idrisi I anatangazwa kuwa Mfalme wa Libya


Bendera ya Libya

[Tarehe 24 mwezi wa 12 mwaka 1951 nchi ya libya inapata uhuru kutoka taifa la Italia]

Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediterania,

inayopakana na Misri,Sudan,Niger,Chad,Algeria,Tunisia.

Nembo ya Libya

Eneo kubwa la nchi ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi.

Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah.

Asili ya Wakazi wa Libya walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.

Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea

Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.

katika karne ya 7 Waarabu Waliingiza Uislamu na utamaduni wao

Mwaka 1551 Waturuki waliwafukuza Wazungu kutoka Tripoli

wakatawala hadi karne ya 20.

Picha ilipigwa january 21 2006, Mji wa Tripoli

Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941.

Waingereza waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji.

Kisha kumpindua mfalme Idris I,

Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011.

Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakazi wa Libya ni mchanganyiko wa Waberberi,Waarabu na Waturuki 74%,

mbali na Waberberi (25%) ambao ndio wakazi asilia, lakini wengi wao wameanza kutumia lugha ya Kiarabu pia.

Kuna pia wahamiaji kutoka nchi za jirani, za kandokando ya Bahari ya Kati na kutoka Bara Hindi.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu