Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mwanaharakati Askofu aliyepinga serikali kuhusu ufukara, dhuluma, mauaji na unyanyasaji katika jamii aliuawa akiwa kanisani

December 22, 2018

Óscar Arnulfo Romero y Galdámez  alizaliwa tarehe 15 Agosti 1917 na kufariki  tarehe 24 Machi  mwaka 1980.

 alikuwa askofu mkuu wa Kanisa Katoliki huko San Salvador, nchini El Salvador kuanzia tarehe 21 Juni 1970 hadi kifo  chake

Baada ya vitisho mbalimbali, Romero aliuawa wakati anapoadhimisha Misa. Ingawa hakuna aliyehukumiwa kwa kumuua

kamati ya Umoja wa Mataifa imethibitisha kwamba aliuawa kwa agizo la mwanasiasa wa mrengo wa kulia Roberto D'Aubuisson.

 Hatimaye mnamo Oktoba 2018 mahakama iliagiza mhusika mmojawapo akamatwe ingawa haijulikani yuko wapi, huenda  alishahama El Salvador.

 Kwa heshima yake, mwaka 2010, Mkutano Mkuu wa UM ulitangaza tarehe 24 Machi kuwa "International Day for the Right to the Truth Concerning Gross Human Rights Violations and for the Dignity of Victims"

Óscar Romero alivyochorwa na J. Puig Reixach (2013)

 

Papa Fransisko alimtangaza mwenye heri tarehe 23 mei 2015 na mtakatifu tarehe 14 oktoba 2018

 Ibada ya kumtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 2015 huko San Salvador.

Anaheshimiwa na Wakristo kadhaa wa madhehebu mengine pia kama mfiadini

 

El Salvador ni nchi ndogo kuliko zote za Amerika ya Kati, lakini yenye msongamano mkubwa zaidi, ikiwa na wakazi 6,290,420 katika km2 21,040.

Imepakana na Guatemala, Honduras na bahari ya Pasifiki.

 Ramani ya El Salvador 

 

Jina la nchi kwa Kihispania linamaanisha "Mwokozi" kwa heshima ya Yesu Kristo, ambapo wananchi wengi ni wafuasi wake katika Kanisa Katoliki (47%)

au katika madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (33%)

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload