Mfahamu mwanaharakati aliyesababisha rais Hosni Mubarak na serikali yake kujiuzulu nchini Misri

December 21, 2018

 Asmaa Mahfouz

 

Asmaa Mahfouz [alizaliwa mwaka 1985]

ni mwanaharakati,mwandishi wa blogu na mwanzilishi  mmojawapo wa Harakati za vijana wa 6 April nchini Misri

Asmaa Mahfouz kwenye Uwanja wa Tahrir, Kairo

 

Mnamo Januari 2011 vijana Wamisri wanne waliwahi kujichoma moto kutokana na kukata tamaa kwa sababu ya hali duni ya nchi na maisha yao

 

Asmaa alitumia blogu yake ya video kupinga udikteta wa rais Hosni Mubarak na hali duni ya haki za binadamu nchini Misri

Alisema, "Wamisri wanne walijichoma kwa kupinga aibu ya udhalilishaji, njaa na umaskini waliopaswa kuishi nazo kwa miaka 30. ... Leo hii mmoja wao amefariki."

 

Akaendelea kuwaambia wananchi, "tuone aibu fulani ... Badala ya kujichoma moto tufanye kitu cha maana.

 Kuketi nyumbani na kufuatilia habari tu kwa TV au facebook itatupeleka penye udhalilishaji

 

Aliita wananchi kukutana kwenye uwanja wa Tahrir mjini Kairo tarehe 25 Januari 2011.

Video yake aliipeleka YouTube ilipoangaliwa na wengi. Video hii iliendelea kuwa ishara ya kuanzisha mapinduzi ya Misri ya 2011.

 Asmaa Mahfouz kwenye Uwanja wa Tahrir, Kairo

 

Siku iliyotajwa kwenye blogu malakhi ya Wamisri walifika uwanja wa Tahrir. Polisi 30,000 walishindwa kuwafukuza, mamia walikamatwa,

 mjini Suez wananchi 2 waliuawa na polisi wakati wa maandamano.

 

Maandamano yalifuatana siku kwa siku hadi kujiuzulu kwa serikali na hatimaye rais Mubarak mwenyewe mnamo Februari 2011

 

Mwezi Agosti mwaka huohuo Asmaa alikamatwa na kushtakiwa mbele ya mahakama ya kijeshi kwa sababu ya kukosoa Kamati Kuu ya Kijeshi iliyowahi kuchukua nafasi ya rais aliyepinduliwa tayari. lakini baadaye Aliachiwa

Mnamo Oktoba 2011 Asmaa Mahfouz aliteuliwa, pamoja na wanaharakati wengine wa Misri, kwa Tuzo ya Sakharov 

 iliyotolewa na na Bunge la Ulaya kwa sababu alitetea haki za binadamu kwa kuwapa Wamisri motisha ya kudai haki zao kwenye uwanja wa Tahrir,

kwa njia ya video na blogu zake kupitia Youtube, Facebook na Twitter.

 Tarehe 14 Desemba 2011 Asmaa alipokea mwenyewe tuzo  katika sherehe maalumu kwenye bunge la Ulaya huko Strasbourg

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon