Rais aliyejulikana kwa amri yake ya kuwa mawaziri na maafisa wote wa serikali yake wasitumie magari

Noel isidore Thomas sankara alizaliwa tarehe 21 desemba mwaka 1949 mjini Yako, Volta ya juu; mjini Quagadougou, Burkina Faso

Thomas Sankara, Rais wa Burkina Faso (1983-1987)

alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa nchini Burkina Faso. Kuanzia 4 Agosti 1983 hadi kuuawa kwake tarehe 15 Oktoba 1987,

Sankara alikuwa rais wa tano wa Volta ya Juu aliyeweza kuibadilishia jina la nchi yake kuwa Burkina Faso.

Sankara alipanda ngazi ya kijeshi hadi cheo cha kapteni. Pamoja na mwanajeshi mwenzake Blaise Compaore alishiriki katika chama cha siri cha "maafisa Wakomunisti" waliolenga kupambana na ufisadi.

Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya rais Jean-Baptiste Ouédraogo na kupandishwa cheo kuwa waziri mkuu kwa miezi michache kuanzia Februari 1983

Mwezi Mei alikamtawa na kutiwa mbaroni. Mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Blaise Compaore yalimfanya kuwa mwenyekiti wa kamati ya mapinduzi na rais wa tano wa Volta ya Juu.

Sankara alibadilisha jina la nchi kuwa Burkina Faso.

Alijulikana hasa kwa amri yake ya kuwa mawaziri na maafisa wote wa serikali yake wasitumie magari makubwa bali gari dogo aina ya Renault 5 ambayo ilikuwa gari la bei ya chini iliyopatikana nchini Burkina Faso

Pamoja na hayo, alishirikisha wanawake wengi katika serikali yake akapiga marufuku tohara kwa wanawake.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu