Kuteswa kwa Wahamiaji na wakimbizi wanaopitia Libya haisemeki.


Mhamiaji akiwa katika kituo cha kuzuiliwa nchini Libya mnamo Februari 1 2017, wakati UNICEF walipotembelea kituo hicho kulikuwa na wanaume 160.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini Geneva Uswisi na Tripoli imesema wahamiaji na wakimbizi wanakabiliwa na hofu na mateso yasiyopimika pindi wanapoingia nchini Libya na

muda wote wanaoishi katika nchi hiyo wakiwa katika harakati zao za kusogea mbele na kujaribu kuvuka bahari ya Mediteranea.

Ripoti hiyo yenye kurasa 61 ikiwa imechapishwa kwa ushirikiano wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na haki za binadamu

imeangazia kipindi cha miezi 20 nyuma hadi kufikia mezi Agosti mwaka huu wa 2018, ikionesha kuwa kuna ukiukwaji mkubwa na manyanyaso yanayofanywa na maafisa wa serikali, makundi yenye silaha, waporaji na wasafirishaji haramu wa wahamiaji na wakimbizi.

Matendo hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu ni pamoja na mauaji, mateso, kuwaweka watu vizuizini, ubakaji, utumwa na kuwafanyisha kazi kimabavu.

Kwa kutumia visa 1300 ambavyo vimefuatiliwa na watu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na kwa wahamiaji ambao wamerejea Nigeria au wamefika Italia,

ripoti inafuatilia safari nzima ya wahamiaji na wakimbizi kutoka mpaka wa kusini wa Libya, kupitia jangwani hadi pwani ya kaskazini, safari ambayo inakabiliwa na hatari kubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kila hatua inayopigwa njiani humo.

Ripoti imeendelea kueleza kuwa wanawake wengi na wasichana waliohojiwa na UNSMIL wameripoti kubakwa na wahalifu, wavamizi na wasafirishaji haramu.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliotembelea vituo 11 ambako maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wanashikiliwa,

walikusanya Ushahidi wa mateso, unyanyasaji, utumikishwaji na ubakwaji unaofanywa na walinzi na wameripoti kuwa wanawake mara nyingi wanawekwa katika maeneo ambayo hakuna walinzi wa kike hali ambayo inaongeza uwezekano wa hatari ya kubakwa na kufanyiwa manyanyaso mengine. Mara nyingi wanawake wanaoshikiliwa hulazimika kufanyiwa ukaguzi wakiwa bila nguo huku wakitizamwa na walinzi wanaume.

Wale ambao wanafanikiwa kujaribu kuvuka bahari ya Mediterania, hukamatwa na walinzi wa Pwani ya Libya na kisha hurejeshwa Libya ambako wanarudishwa katika mateso waliyoyatoroka.

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu Michelle Bachelet akizungumzia kinachoendelea nchini Libya amesema, “Hali hiyo ni mbaya na ya kutisha

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu