FAO yainua wakulima wadogo wadogo Tanzania kwa kuwapa stadi za kilimo.


Shirika la Chakula na kilimo duniani FAO kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wameungana kutelekeza mradi wa kuwafundisha wakulima wadogowadogo stadi za kilimo bora.

Tayari zaidi ya wataalam 1000 wanaofanya kazi katika wilaya zaidi ya 137 nchini Tanzania wamefundishwa stadi hizo katika Chuo cha wakulima cha Mkindo kilichoko Morogoro.

chuo hiki cha wakulima Mkindo mkoani Morogoro kilianzishwa mwaka 1996 kupitia ushirikiano wa Tanzania, FAO na Indonesia chini ya mpango wa ushirikiano wa nchi za kusini

Mashamba darasa ya mwanzo yalitumika kuanzisha aina mpya ya mpunga na teknolojia ya umwagiliaji ili kuongeza wastani wa uzalishaji wa mchele nchini Tanzania kutoka tani 2 hadi 6 kwa hekta

Dkt. Moses Temi wa Chuo cha wakulima Mkindo anasema,“Tulipoanzisha mafunzo hapa miaka 16 iliyopita, tulianza na wakulima 100 ili waongeze uzalishaji na pia wawafundishe wakulima wengine katika Kijiji hiki na pia katika vijiji jirani.

Idadi ya sasa ya wakulima tulio nao ni elfu tatu ambao wanazalisha tani 6 hadi 7 kwa hekta.

Muundo huu umechukuliwa na serikali kama mafanikio na umehusishwa katika programu mbalimbali za kilimo.

Zaidi ya wataalamu 1000 wa kilimo wamepata mafunzo tangu kuanzishwa kwa chuo hiki na ni wataalamu kutoka ngazi ya kijiji hadi taifa.

Takribani kila wilaya nchini Tanzania ina mtaalam mmoja aliyepata mafunzo kutoka Chuo cha wakulima cha Mkindo

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu